
Les Tanzaniens CS.Simba jurer de ne pas retourner à Kinshasa joue acause trouble Motema Pembe partisans et ils ajoutent en disant que le gouvernement tanzanien devrait prendre des mesures pour les Congolais vivant en Tanzanie sans document
MWENYEKITI wa Simba, Ismail Aden Rage, ameapa kwamba timu hiyo haitakanyaga Kinshasa milele na wakipangiwa watajitoa kwani si sehemu salama na amesema watashtaki kwa Serikali ya Tanzania.
Simba ilifungwa mabao 2-0 juzi Jumapili katika mechi ya Kombe la Shirikisho dhidi ya DCMP ya hapa na kuondoshwa katika mchezo huo uliogubikwa na fujo za kila aina ndani na nje ya uwanja.
Baada ya mchezo huo, maelfu ya mashabiki walivamia uwanja kwa lengo la kuidhihaki Simba jambo ambalo lilifanya askari wa usalama kuwatuliza wachezaji na viongozi kwenye benchi la ufundi na kuwazunguka kuwaepusha na fujo hizo zilizodumu mpaka usiku.
Dakika chache baadaye wachezaji hao walisindikizwa tena hadi vyumba vya kubadilishia nguo na kutulizwa kwa zaidi ya saa moja hadi hali ilipotulia, lakini hata mitaani askari walitumia nguvu za ziada na vitisho vya hapa na pale kufungua njia ingawa bado walikuwa wabishi.
Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage alisema; "Wametufanyia mambo mabaya sana, hizi ni hujuma ambazo hazivumiliki, ndiyo maana nasema Simba haitakanyaga milele Kinshasa.
"Hatutakuja kucheza mechi yoyote hapa kwa vurugu hizi, tutagawa pointi za bure. Labda Serikali itoe tamko na tupewe ulinzi maalumu au tucheze nje ya hapa. Na tutakwenda kushtaki Wizara ya Mambo ya Nje kuhusu unyama tuliofanyiwa hapa Kinshasa.
"Tungeshinda tusingetoka hapa uwanjani, wangetuua hawa," alisisitiza kiongozi huyo, ambaye amependekeza ianzishwe vita dhidi ya raia wote wa DR Congo wanaoishi nchini kinyume cha sheria

.
Simba iliwasili jijini Dar es Salaam jana Jumatatu, saa 12.45 jioni kwa ndege ya KQ.
http://www.mwanaspoti.co.tz/wcreadnews.php?id=7303