Un autre Club"Villacher Sportverein" vien de donnee 500 Millon Sh pour ke transfert de Mbwana Samata au momment ou le TP.Mazembe epesaki bango"Simba" 150 Millon Sh
Klabu Ulaya yamtaka Samatta kwa Sh 500m
Mshambuliaji wa timu ya Simba na Taifa Stars Mbwana Samatta katikati akipongezwa na wenzake
MWANDISHI WETU
KLABU ya Villacher Sportverein ya Austria imewaambia Simba kuachana na Shilingi milioni 150 za TP Mazembe kwani wao wanamtaka Mbwana Samatta kwa Shilingi milioni 500.
Barua iliyoandikwa na klabu hiyo ya Ligi Kuu Austria, Jumatano iliyopita inasema kuwa inamkaribisha Samatta kufanya majaribio na klabu hiyo kwa siku 30.
"Tumevutiwa na mchezaji wenu kinda anayekuja kwa kasi katika soka, tunaomba aje kufanya majaribio kwa siku 30. Tutampa viza, malazi, chakula na huduma zote za afya akiwa hapa," inasema barua hiyo iliyoandikwa na Rais wa Villacher, Egon Putzi.
Faida nyingine ya klabu hiyo huenda msimu ujao ikashiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya au Ligi ya Europa kutegemeana na nafasi itakayomaliza nayo kwenye Ligi Kuu Austria.
Klabu hiyo imesema iwapo Samatta atafanikiwa majaribio itamnunua kwa Simba kwa Euro 200,000 (Shilingi milioni 500 za Tanzania) pamoja na kumpa mshahara mkubwa.
Klabu nyingine ambayo imetuma mwaliko kwa Samatta ni Stabaek ya Norway.
Katika barua yao ya Aprili 11, klabu hiyo inamtaka Samatta kwenda Norway kuanza mazoezi Juni Mosi.
Barua hiyo ambayo imeandikwa na Mkurugenzi wa Michezo wa klabu, Inge Andre Olsen inasema kuwa Samatta atafanya mazoezi mpaka mwisho wa Julai.
Kama hiyo haitoshi, klabu nyingine ya Sporting Lisbon ya Ureno, imeendelea kumtaka Samatta aende kufanya majaribio.
Mmoja wa mawakala maarufu duniani, Marco Guimaraes amesema Samatta anahitajika kwenda kufanya majaribio mwezi Juni katika klabu hiyo na kuwa mambo mengine yatajulikana akifuzu.
Wakati TP Mazembe ikitaka kuwalipa Simba Dola 100,000 (Sh.150m), timu ya Austria inayoshika nafasi ya pili katika Ligi Kuu itailipa Simba mara tatu zaidi ya kipato ambacho Wacongo wanataka kumpa.
Katika hatua nyingine, TP Mazembe imeshindwa kutuma mkataba wa Samatta kwa mwanasheria wake, Damas Ndumbaro.
Ndumbaro aliwaandikia barua pepe TP Mazembe Aprili 16 kutaka watume mkataba kati ya klabu hiyo na Samatta, lakini hawajatuma.
"Hawezi kusaini mkataba kwa sababu mwanasheria wake, ambaye inabidi nimshauri bado sijauona mkataba huo. Nasuburi wanitumie ndipo tujue tutaanzia wapi," alisema Ndumbaro kwa kifupi jana Ijumaa.
Habari za ndani zinadai kuwa TP Mazembe wanataka kumsainisha mkataba wa miaka mitano kinyume na taratibu za Fifa, ambazo kwa mchezaji wa umri wa Samatta, mkataba mrefu kabisa ni wa miaka mitatu.
http://www.mwanaspoti.co.tz/wcreadnews.php?id=6537